Ethiopia yakosolewa kwa kufanya udukuzi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn

Shirika la kutetea haki za binadamu la Huma Rights Watch limeituhumu serikali ya Ethiopia kwa kuwapeleleza wapinzani wake.

Kwa mujibu wa shirika hilo, serikali hunasa mawasiliano yao kupitia kwa simu zao za mkononi au kompyuta zao.

Shirika hilo limesema kuwa maafisa wa utawala Ethiopia wamenunua programu na vifaa vya kunasa mawasiliano kutoka Ulaya na nchini China , katika mpango wake wa kukandamiza wapinzani.

Raia wa Ethiopia wanaoishi Uingereza na nchini Marekani pia wameituhumu serikali mjini Addis Ababa kwa kutumia programu hizo kunasa mawasiliano katika kompyuta zao.

Waziri wa mawasiliano wa Ethiopia amekanusha madai hayo.

Hata hivyo shirika hilo limesema kuwa liliwahoji zaidi ya watu miamoja ikiwemo majasusi wa zamani.