Miili ya watu 15 yapatikana CAR

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Vita vimeendelea kutokota nchini humo licha ya Rais wa muda kuchukua usukani

Shirika la msalaba mwekundu Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati linasema kuwa limefanikiwa kupata miili ya watu 15 ambao wameauwa tangu siku ya Jumamosi.

Miili hiyo ilipatikana katika eneo la kibiashara la mji wa Bangui linalojulikana kama PK-5 ambapo maelfu ya waislamu wanadaiwa kukwama.

Ghasia zilizuka katika eneo hilo mwishoni mwa juma kati ya waislamu na wakristo wanaojiita Anti-Balaka.

Ni mwaka mmoja tangu waasi wamuondoe aliyekuwa rais wa taifa hilo Franswa Bozize hatua iliosababisha maafa makubwa kati ya waislamu na wakristo.