Watu 4 waambukizwa Ebola Conakry

  • 28 Machi 2014

Watu wanne wamethibitishwa kuugua ugonjwa hatari wa Ebola katika mji mkuu wa Guinea,Conakry.

Image copyright
Image caption Ni mara ya kwanza kwa Ebola kuzuka Conakry

Wataalamu wa afya wamesema kuwa wamewatenga wanne hao katika wadi ya hospitali moja mjini humo. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Ebola kuzuka mjini humo.

Tangu kuzuka kwa homa hiyo hatari mwezi uliopita, zaidi ya watu sitini wamefariki nchini humo.

Ripoti hizo zinajiri siku moja tu baada ya wataalamu wa afya nchini Guinea kusema kuwa homa hiyo hatari ilikuwa imedhibitiwa katika mkoa wa kusini.

Hata hivyo, kuenea kwa Ebola mjini Conakry kunadhirisha changamoto katika vita dhidi ya ugonjwa huo kutokana watu kusafiri kutoka eneo moja hadi lingine .

Nchi jirani zimeimarisha huduma zao za afya hasa katika maeneo ya mipakani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii