Suluhu kwa mzozo wa Crimea.

Haki miliki ya picha y
Image caption Obama akitoa hotuba yake huko Brussels kuhusu mustakaballi wa Crimea

Rais Barack Obama ameitaka Urusi kujua kwamba haitapata usalama na maendeleo kupitia njia ya dhulma baada ya kunyakua jimbo la Crimea.

Katika Hotuba yake huko Brussels Ubelgiji, Bwana Obama amesema Marekani na Uropa haina haja ya kuchukua udhibiti wa Ukraine.

Amezitaka nchi wanachama wa muungano wa NATO kuchukua jukumu la kusuluhisha mzozo kuhusu umiliki wa eneo la Crimea.

Rais Obama ameionya Urusi kuwa iwapo itaendelea kushikilia msimamo wake basi itazama katika vikwazo vikali zaidi.

Kwa upande wake Urusi inaendelea kusisitiza kwamba ilifuata utaratibu unaokubalika kimataifa katika kuandaa kura ya maoni kuamua iwapo eneo la Crimea linapaswa kumilikiwa na Urusi au Ukraine.

Wakati huohuo wajumbe wa Ukraine walioko London kwa mazungumzo na serikali ya Uingereza, wameiomba Uingereza kufanya kila jitihada kujaribu kuilinda Ukraine kutokana na tamaa mbaya ya Urusi.