Thai imegundua vifusi 300 baharini

Image caption Picha za setlaiti ya Thai inayoonesha vifusi kwenye bahari Hindi

Shirika la anga za juu nchini Thailand linasema kuwa mtambo wake wa satelite umetambua vifusi zaidi ya mia mbili vikielea katika eneo la kusini mwa bahari Hindi ambako ndege iliyopotea ya shirika la

ndege la Malaysia MH370 ilitoweka.

Kwa mjibu wa afisa wa Anond Snidvongs, kutoka kituo hicho utabiri na anga za juu ,Vifusi hivyo vinaripotiwa kuwa na urefu wa kati ya mita mbili hadi kumi na tano na vilionekana takriban kilomita 200

kutoka kwenye eneo lililopigwa picha na setlaiti ya Ufaransa.

Mtambo wa satelite unaomilikiwa na Ufaransa ulikuwa umetambua takriban vifusi mia mbili ishirini ambavyo huenda vilitoka kwenye ndege hiyo ya MH370 iliyotoweka.

Awali operesheni ya kuitafuta ndege hiyo katika eneo la kusini mwa bahari Hindi iliahirishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Mjini Beijing, katika mkutano wa maswali na majibu kati ya watu wa familia za abiria wa ndege hiyo na maafisa Luteni kanali Ackbal Abdul Samad wa jeshi la Malaysia alisema kuwa lengo kuu kwa sasa ni

kutafuta kisanduku cha habari cha ndege hiyo (blackbox).