IMF kuipa Ukraine dola bilioni 10

Haki miliki ya picha Getty
Image caption IMF yakubali kuisiadia Ukraine

Shirika la fedha duniani IMF limesema kuwa litaipa Ukraine mkopo wa kati ya dola bilioni kumi na nne na na kumi nane.

Makubaliano ambayo bado yanasubiri kuidhinishwa na bodi ya IMF na yanatarajiwa kuwa mwanzo wa misaada zaidi ya kimataifa.

Muungano wa Ulaya, Marekani na Japan nao wanatarajiwa kuongeza msaada zaidi kwa Ukraine.

Tangazo hilo linajiri baada ya Ukrain kusema kuwa itaongeza gharama ya gesi inayotumiwa nyumbani kwa asilimia hamsini.

Hiyo ni moja ya mashartii iliyowekewa serikali ya mpwito ya Ukraine kabla ya kupewa msaada huo.

Aliyekuwa rais wa taifa hilo Viktor Yanukovich alikuwa amekataa kata kata kuongeza bei ya bidhaa hiyo muhimu lakikni Waziri mkuu mpya Arseny Yatsenyuk ameitahadharisha bunge la taifa hilo kuwa

hawana budi kuongeza bei ya gesi ilikunusuru uchumi wa nchi hiyo .

Ukraine imekuwa ikitegemea gesi nafuu kutoka kwa kampuni kubwa ya gesi ya Urusi Gazprom na tayari Urusi imesema kuwa ruzuku hiyo itaondolewa ifikapomwisho wa juma lijalo.

Wadadisi wanasema kuwa uchumi wa Ukraine utadorora kwa takriban asilimia 10% katika kipindi cha mwaka mmoja ujao kutokana na jitihada za kupunguza kutegemea kwake kwa Urusi .

Aidha kampuni ya gesi ya Naftogas linanakisi ya bajeti ya takriban asilimia 2% ya bajeti ya Ukraine.