MH370;Ndege ya New Zealand imeona vitu

Juhudi za kutafuta mabaki ya ndege ya Malaysia MH370: iliyotoweka mapema mwezi huu ikiwa na abiria 239 imepigwa jeki na kuonekana kwa vitu kadha vikielea kwenye eneo lililotangazwa kuwa lengwa .

Tayari ndege ya jeshi la New Zealand imeripoti kuona vitu 11 vikielea katika eneo lililoko takriban kilomita 1,100km mashariki mwa eneo lililokisia kuwa ndege hiyo ilianguka.

Hata hivyo maafisa wa shirika linaloongoza shughuli hiyo ya kuitafuta ndege hiyo MH370 wamesema kuwa vitu hivyo vilivyoonekana vitadhibitishwa kesho kutokana na umbali wa eneo hilo lipya .

Mwandishi wa BBC aliyeko Perth Australia amesema ripoti hiyo ni ya kuaminika zaidi ya picha za mitambo ya setlaiti ambazo zimekuwa zikiwapotosha .