Polisi Misri wakabili waandamanaji

Image caption Maandamano Misri

Polisi nchini Misri wanaripotiwa kuwarushia vitoa machozi waandamanji wanaliunga mkono kundi lililopigwa marufuku la Musllim Brotherhood.

Vyombo vya habari vya serikali vilisema kuwa waandamanaji waliokuwa wakilishutumu jeshi walikusanyika kusini mwa mji wa Cairo baada ya maombi ya siku ya Ijumaa.

Walinda usalama zaidi wamepelekwa mjini Cairo baada ya wito kutoka kwa kundi la Muslim Brotherhod kwa wafuasi wake wa kuwataka kufanya maandano ya kupinga uamuzi wa aliyekuwa mkuu wa majeshi Abdel Fattta al- sisi kuwania urais nchini Misri.

Misri imekumbwa na manadamno na ghasia tangu kuondolewa madarakani kwa rais Mohammed Mosri mwaka mmoja uliopita.