Obama azuru Saudi Arabia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Obama azuru Saudi Arabia

Rais Obama anazuru Saudi Arabia kwa ziara ambayo Marekani itaihakikishia Saudia kwamba ndiye mshirika wake mkubwa katika eneo hilo la mashariki ya kati.

Ziara hii wadadisi wa maswala ya kidiplomasia wanasema inafuatia kudorora kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya kiusalama anasema kuwa uhusiano kati ya serikali hizo mbili umezorota ikilinganishwa na wakati mwengine wowote.

Saudi Arabia imeshtumu sera za Marekani katika eneo la mashariki ya kati ,ikiwemo kushindwa kwa Obama kuichukulia hatua za kijeshi serikali ya Syria.

Vilevile taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta lina wasiwasi kuhusu kuimarika kwa uhusiano kati ya marekani na Iran mbali na sera za marekani nchini Misri.