Jamaa wa abiria wataka ukweli Malaysia

Jamaa wa abiria wa ndege ya Malaysia iliyopotea Haki miliki ya picha Reuters

Jamaa kama 30 wa abiria wa Uchina waliotoweka na ndege ya Malaysia wamesafiri hadi Kualu Lumpur, mji mkuu wa Malaysia, kuwahimiza wakuu wajibu maswali yao.

Walitoa bango katika uwanja wa ndege wakisema wanataka ushahidi na ukweli kuhusu nini kimesibu ndege hiyo.

Wanataka wakuu wa Malaysia waombe msamaha kwa kusema kuwa ndege hiyo imepotea katika Bahari Hindi na kwa kuchelewa kutoa habari hizo.

Mwandishi wa BBC amesema kuwa kuwasili kwao kulizua hali ya wasiwasi na familia hizo zilipewa ulinzi mkali na watu wa Malaysia waliojitolea, na hivyo kuwa vigumu kwa waandishi wa habari kuwafikia.