Vidhibiti mwendo ni lazima Kenya

Image caption Ajali ya barabarani Kenya

Maelfu ya madereva wa uchukuzi wa umma nchini Kenya wamekua na wakati mgumu kuhakikisha magari yao yanazingatia sheria mpya na kali za barabarani ifikapo Jumanne ya wiki hii.

Sheria hii inashurutisha wahudumu wa magari yote ya abiria kuweka vidhibiti mwendo vya kisasa ambavyo vitazuia ajali nyingi za barabarani.

Taarifa inasema ni magari machache sana yaliyowekwa vidhibiti mwendo hivyo ambavyo wizara ya uchukuzi imesema kuwa magari yasiyokuwa navyo hayataruhusiwa barabarani.

Waakilishi wa sekta ya usafiri wa umma, wameitaka serikali kuwaongeza muda madereva ambao wamekosa kupata vifaa hivyo , ingawa mahakama ilitupilia mbali ombi lao.

Abiria wana wasiwasi kwamba huenda wakakumbwa na changamoto ya usafiri siku ya Jumanne kutokana na uhaba wa magari yaliyowekwa vidhibiti hivyo.

Pia kuna hofu kuwa huenda yakapandisha nauli.

Hatua hii imechukuliwa na serikali ili kupunguza ajali za barabarani.

A BBC correspondent in the Kenyan capital Nairobi says commuters are worried there will be a public transport crisis on Tuesday. (The regulations are designed to reduce carnage on the roads.)