Zuma:'Sikuagiza ukarabati wa nyumba'

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nyumba ya Zuma iliyokarabatiwa

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema hadhani ni sawa kurejesha fedha za umma zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafsi kwa sababu hakuwahi kutoa pendekezo hilo.

Bw. Zumaamesema haoni haja ya kuchangia pesa zake binafsi katia ukarabati wa nyumba hiyo kwani halikuwa pendekezo lake toka mwanzoni.

Kadhalika bwana Zuma ameambia runinga moja nchini Afrika Kusini kwamba maafisa wa serikali ndio waliopanga ukarabati huo uliogharimu dola milioni 23 bila kumuarifu.

Hii ndio mara ya kwanza Rais Zuma amezungumzia kuhusu makaazi hayo yaliyozua mjadala mkali wa umma Afrika Kusini.

Mhifadhi wa mali ya umma alisema baadhi ya ukarabati uliofanywa sio halali na kumtaka Zuma kurejesha baadhi ya fedha zilizotumika.