Hoja:Je usawa wa kijinsia unaweza kufikiwa?

Je kuwa msichana au mwanamke kunakuzuia uhuru wa kufanya mambo mengi unayoyataka?

Hakuna nchi hata moja moja duniani ambako wanaume na wanawake wana haki sawa kulingana na utafiti mwingi uliofanywa kuhusu maswala ya usawa wa kijinsia.

Hii ni licha ya nchi nyingi duniani kuwa na sheria pamoja na mifumo ambayo pakubwa imebuniwa kuwapa wasichana na wavulana , wanaume kwa wanawake nafasi sawa katika jamii.

Sasa je nini kizingiti kikubwa katika kuhakikisha kuwa usawa huu unafikiwa?

Tupe maoni yako kupitia ukurasa wetu wa Facebook https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209 na Twitter @bbcswahili

Hii ni sehemu ya makala ya BBC kuhusu uhuru mwaka 2014