Mkuu wa polisi auawa nchini Misri

Haki miliki ya picha
Image caption Mashambulizi dhidi ya polisi Misri yamekuwa yakiongezeka

Brigedia Jenerali wa jeshi la polisi nchini Misri ameuawa katika milipuko miwili tofauti iliyotokea kwa wakati mmoja karibu na chuo kikuu cha Cairo.

Vyombo vya habari vinasema kuwa watu wengine wanne walijeruhiwa katika mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, mabomu yalikuwa yametegwa karibu na kituo cha polisi.

Hauna kundi lolote limekiri kufanya mashambulizi hayo.

Misri imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya taasisi za serikali yanayofanywa na makundi ya wapiganaji hasa baada ya kupinduliwa kwa aliyekuwa Rais Mohammed Morsi mwezi Julai.