Wanajeshi wa Chad kuondoka CAR

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Chad walikwenda Bangui kusaidia wanajeshi wa Muungano wa Afrika kushika doria

Chad imeamua kuondoa wanajeshi wake kutoka katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Wanajeshi hao wamekuwa nchini humo kwa miaka mingi.

Zaidi ya wanajeshi 850 wamekuwa wakisaidia kikosi cha muungano wa Afrika kinachoshika doria nchini humo.

Lakini wamekosolewa kwa kuunga mkono waasi wa kundi la kiisilamu la Seleka.

Waziri wa mambo ya nje wa Chad amesema kuwa licha ya wanajeshi wake kujitolea kusaidia hali nchini CAR, wamekuwa wakituhumiwa kwa kupendelea upande mmoja na kuchochea hali nchini humo.

Taifa hilo la Magharibi mwa Afrika limekumbwa na mgogoro wa kidini tangu waasi kuchukua mamlaka mwaka jana.