Katika Teknolojia wiki hii:

Haki miliki ya picha BBC World Service

Kampuni ya Amazon imezindua televisheni yake inayotumia Internet. Imeundwa kushindana na kampuni za Apple na Google.

Televisheni hiyo itawawezesha watumiaji wake kupokea taarifa moja kwa moja kutoka katika maktaba ya Amazon, pamoja na huduma nyinginezo wanazotaka.

Kwa jina Amazon Fire TV, watumiaji pia wanweza kucheza michezo kwenye mitandao.

Tayari inauzwa nchini Marekani kwa dola 99.

Mpango mkubwa zaidi wa kutazama na kuchunguza ardhi kutoka angani kwa kutumia mtambo wa Satelite wa Eu,umezinduliwa.

Mtambo huo unaojulikana kama, Craft, utafuatwa na mitambo mingine ya Satelite yote ambayo inaweza kurusha data na vipimo vya sayari ya Ardhi kutoka angani.

Mradi huo unatarajiwa kutoa maelezo zaidi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kusaidia kutathmini uwezekano wa kutokea majanga.

Ni wakati wa mashindano ya sauti kuanza sasa! Kampuni ya Microsoft imezindua kifa cha Cortana, jibu lake kwa Siri, kitakachotumika kwa simu ya mkononi ya Windows.

Kifaa hicho cha sauti kimepata jina lake kutokana na (AI) katika mchezo wa Halo na kinatumia programu ya Microsoft Bing, ya tafuta tafuta kuweza kufanya kazi kwa kuamrsihwa.

Microsoft pia imetangaza programu mpya ya Windows, 8.1 itakayopewa watumiaji wa microsoft bila malipo.

Na hatimaye, sahau uwezo mkubwa wa kupiga picha kwa simu yako au kwenye TV.

Kutana na Pixelbots.

Hii ina uwezo mara 75 wa kuweza kuunda picha ndogondogo kwenye tabiti na whiteboards.

Kwa hivyo wakati unapoogopa robo-pocalypse, usiwe na wasi wasi maana itakuwa na sura nzuri