Rwanda miaka 20 baadaye nini kimebadilika?

Image caption Watu wakitoroka mauaji ya kimbare Rwanda mwaka 1994

Katika muda wa siku mia moja kati ya mwezi Aprili na mwezi Juni mnamo mwaka 1994, Watu takriban laki nane waliuawa katika mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Athari za Maafa ya mauaji ya kimbari zilikushuhudiwa nchini Rwanda na katika nchi Jirani.

Miaka ishirini baadaye Ukanda wa maziwa makuu umewezaje kukabiliana na yaliotukia?

Idhaa ya Kiswahili ya BBC itakuletea matangazo maalum kila siku moja kwa moja kutoka Kigali kuanzia Jumatatu Tarehe 7 Aprili hadi Ijumaa tarehe 11 Aprili.

Kilele cha matangazo hayo utakuwa mjadala ambapo tutakuwa tunauliza Je Afrika iko tayari kuzuia mauaji kama yaliyotokea Rwanda miaka ishirini iliyopita?

Anza kuchangia maoni yako kuhusu hali nchini Rwanda kupitia ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/pages/BBC-Swahili/160894643929209

na Twitter @bbcswahili