Urusi yatoa onyo kali kwa Ukraine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanaharakati wanaopendelea Urusi kutoka Ukraine

Urusi imeionya Ukraine kuancha maandalizi yoyote ya kijeshi kusini na mashariki mwa nchi hiyo, ikisema kwa kufanya hivyo kutaanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi imesema Ukraine ilikuwa ikipanga kupeleka majeshi yake katika maeneo hayo, ikituhumu kwamba makandarasi binafsi wa kijeshi wa Marekani ni miongoni mwa watu waliokuwa katika mpango huo.

Onyo la Urusi limekuja baada ya serikali ya Ukraine kusema kwamba wanaendesha operesheni dhidi ya ugaidi wakati wa usiku katika jengo la utawala katika mji wa mashariki ya Ukraine wa Kharkiv na kuwakamata watu sabini wanaoiunga mkono Urusi ambao waliliteka jengo hilo. Jumatatu, wanaharakati wanaopendelea kujiunga na Urusi kutoka majimbo ya Kharkiv na Donetsk wametangaza kujitenga na Ukraine. (Urusi imekanusha kuchochea kukosekana kwa utulivu na mawazo ya kujitenga kwa maeneo nchini Ukraine.)