Demba Ba ainua Chelsea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mourinho awahimiza Chelsea wamakinike

Bao la dakika za lala salama za mchezaji wa akiba Demba Ba ilitosha kuifikisha Chelsea katika hatu ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya Chelsea ilipoilaza Paris St-Germain mabao 2-0

katika mechi ya marudiano iliyochezwa katika uwanja wa Stamford Bridge Uingereza.

Bao hilo lilitibua shangwe kutoka kwa kocha Jose Mourinho.

Chelsea ilikuwa imelazwa mabao 3-1 na PSG katika mkondo wa kwanza na ilikuwa hainabudi kufunga mabao 2-0 ilikufufua matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya nusu fainali ya mchuano huo wenye kitita kikubwa zaidi barani.

Hata hivyo mechi hiyo ilivyoanza kwa msisismko mkubwa ilisababisha kujeruhiwa kwa Eden Hazard mapema kunako dakika ya 17 ya mechi hiyo.

Mourinho alimchezesha Andre Schurrle ambaye hakukawia kabla ya kufunga bao la kwanza na kufufua matumaini ya the Blues kutinga nusu fainali.

Mourinho, alitimuka mbio nje ya uwanja na kukatiza sherehe ya wachezaji wake waliokuwa wakimshangilia Ba na kuwahimiza wamakinike ilikuhakikisha wanafuzu kwa mkondo ujao sawia na hali

ilivyokuwa mwaka wa 2004 Porto ilipoilaza Manchester United Old Trafford.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andre Schurrle asherehekea bao la kwanza

Kocha wa PSG Laurent Blanc,alisalia kinywa wazi asijue kilichotokea Stamford Bridge kwani hata mchezaji wa kutegemewa Edinson Cavani hakuweza kuongoza kikamilifu mashambulizi baada ya mchezaji wao wa kutegemewa Zlatan Ibrahimovic kukosa kucheza mechi hiyo.

Kwa ''the special one'' hii itakuwa ni mechi yake ya tatu ya nusu fainali ya kombe la mabingwa barani Uropa akiwa mkufunzi wa Chelsea japo alishindwa katika fursa zake za kwanza mbili na Liverpool.

Chelsea sasa wamefuzu kwa pamoja na Real Madrid iliyoshindwa na Borussia Dortmund 2-0.

Real iliyokuwa ikicheza bila ya nyota wake Christiano Ronaldo ilishinda mkondo wa kwanza 3-0.

Droo ya nusu fainali itafanyika ijumaa.