Ukraine: saa 48 kuamua mustakabal wake

Image caption Majengo yaliyotekwa mashariki ya Ukraine

Waukraine wanaoishi mashariki mwa taifa hilo wanatakriban saa 48 kuamua mustakabal wao la sivyo wakabiliane na vyombo vya usalama vya dola.

Waziri wa masuala ya ndani nchin Ukrain Arsen Avakov amewaambia waandishi wa habari mjini Kiev kuwa hali iliyo mashariki mwa nchi itatatuliwa kstika masaa 48 yajayo aidha kwa mazungumzo au kwa

kutumia nguvu.

Wanaharakati wanaoiunga mkono Urusi bado wameyateka majengo ya serikali kwenye miji miwili iliyo mashariki mwa Ukrain

Duru zinaarifa kuwa baadhi ya waandamani ambao walikuwa wameteka majengo ya serikali katika mji wa Luhansk wameondoka .

Mapema juma hili utawala nchini Ukrain uliendesha kile ulichokiita kampeni dhidi ya ugaidi ukilenga makundi yaliyotenga.

Ukrain inaishutumu Urusi kwa kuchochea ghasia.

Maafisa wa ngazi za juu kutoka Urusi, Marekani , Ukrain na Jumuiya ya Ulaya wamekubalina kufanya mazunguzmo juma lijalo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Majengo yaliyotekwa Donetsk

Mazungumzo hayo yanalenga kuleta uwiano baada ya Urusi kuteka eneo la Crimea mwezi February .

Majeshi ya Urusi yangali karibu na mpaka wa Ukraine .

Taharuki imetanda mijini Luhansk, Donetsk na Kharkiv tangu watu wanaounga mkono hatua ya Urusi kuchukua Crimea kudai wanataka Urusi itawale miji hiyo iliyoko mashariki mwa Ukraine.

Serikali ya Kiev tayari imewataja kuwa magaidi na kuwa inapanga operesheni dhidi ya magaidi hao katika kipindi cha siku mbili zijazo.

Bwana Avakov amesema kuwa afua ni mbili mazungumzo ya amani ama vita.

Kiongozi wa waandamani mjini Luhansk amemuaomba rais wa Urusi Vladimir Putin kuwasaidia wasidhulumiwe na Kiev.

Wakati huohuo serikali ya Kiev imetangaza kuwa imewaachia watu 56 waliokuwa wamekamatwa kwa kuvamia majengo ya Umma.

Huko Kharkiv viongozi wa maandamano wamelaumu serikali ya Kiev kwa matatizo mengi yanayowakumba na wakaitisha kura ya maoni ya kuamua iwapo wangependa kusalia Ukraine ama kujiunga na Urusi.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kiev imetwaa majengo yaliyokuwa yametekwa na waandamanji ingawaji hali ingali tata katika mji ulioko karibu wa Donetsk.