Ukraine yawatuliza wanaotaka kujitenga

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Waziri Mkuu wa mpito wa Ukraine Arsenity Yatsenyuk

Waziri Mkuu wa mpito wa Ukraine Arsenity Yatsenyuk amewaambia viongozi wa eneo la mashariki mwa nchi hiyo kwamba amekusudia kuwaongezea madaraka zaidi kwenye eneo hilo.

Hata hivyo hajafafanua ni kwa kiasi gani atawapa mamlaka hayo na kwamba madaraka hayo kama yanaweza kuwaridhisha wakazi wa eneo hilo lenye viwanda la Mashariki mwa Ukraine ambalo linataka kujitenga.

Bwana Yatsenyuk ameutembelea mji wa Donetsk katika jitihada zake za kushughulikia msimamo wa waandamanaji wanaounga mkono Urusi ambao wameteka majengo ya serikali za mtaa na kutangaza uhuru kutoka nchi ya Ukraine.

Wanaharakati pia wameendelea kushikilia majengo ya serikali katika mji wa Luhansk.

Tayari Ukraine imeishutumu Urusi kwa kuchochea uvunjifu wa amani nchini Ukraine.