Morocco yafyeka kikundi cha al-Qaeda

Wapiganaji wa ISIS nchini Syria Haki miliki ya picha AP

Morocco imetangaza kuwa inakifyeka kile ilichoeleza kuwa kikundi kipya cha magaidi ambacho kinaajiri watu wa kwenda kupigana Syria.

Katika taarifa yao, polisi wa Morocco walisema kuwa kikundi hicho kilishirikiana na waakilishi wa mashirika yaenye uhusiano na al-Qaeda kama "taifa la Kiislamu la Iraq na Mashariki ya Mediterranean", ISIS, na kundi la al-Nusra Front.

Polisi walisema kikundi hicho cha Morocco kiliwapatia mafunzi vijana kabla ya kuwatuma kupigana nchini Syria, na kwamba kinakusanya fedha kugharimia safari hizo za kuwapeleka Syria.

Mkuu wa mashtaka wa Morocco ameanzisha uchunguzi.