Wafuasi wa Urusi Ukraine wateka kituo

Waandamanaji wanaounga mkono Urusi katika mji wa Donetsk, mashariki mwa Ukraine Haki miliki ya picha Reuters

Nchini Ukraine, watu wasiojulikana wameliteka jengo la idara ya polisi katika mji wa Slaviansk, mashariki mwa Ukraine.

Msemaji wa polisi katika eneo hilo, Ihor Dyomin, aliiambia televisheni ya Ukraine kwamba washambuliaji walikuwa na silaha kamili na walitumia moshi wa kutoza machozi:

"Watu wasiojulikana waliovaa nguo za jeshi, wamelivamia jengo la utawala la polisi katika mji wa Slaviansk.

Hawakutoa madai yoyote bado.

Tunajaribu kuchunguza sababu na lengo lao.

Ni watu kama 15 hadi 20 wenye silaha; wamo ndani ya jengo hilo.

Waliwaambia wafanyakazi wa polisi hapo wende nyumbani na maafisa waliokuwa zamu tu ndio waliobaki.

Jengo hilo lilitekwa haraka wakitumia moshi wa kutoza machozi.

Wafanyakazi wawili-watatu walipaliwa na moshi waliotumia washambuliaji hao."