Mahakama yamuadhibu Silvio Berlusconi

Haki miliki ya picha .
Image caption Silvio Berlusconi

Waziri mkuu wa zamani wa Italia, Silvio Berlusconi, amepewa kifungo cha nje na kushuritishwa kufanya kazi ya kuhudumia jamii kwa mwaka mmoja.

Mahakama moja mjini Milan imetoa adhabu hiyo kwa Barlusconi kutokana na kesi yake ya kukwepa kulipa kodi.

Mahakama ya juu zaidi ilikuwa imemhukumu jela Berlusconi lakini kwa sababu ya umri wake alitakiwa kuchagua kati ya huduma kwa jamii na kifungo cha nyumbani.

Mawakili wa Berlusconi walimuombea adhabu ya kufanya kazi na kuhudumia jamii na mahakama ikakubali.

Berlusconi mwenye umri wa miaka 77 tayari amepigwa marufuku kugombea katika uchaguzi mkuu kwa miaka sita.

Alipatikana na hatia ya kosa hilo katika kashfa iliyohusu ununuzi wa haki miliki ya televisheini katika kampuni yake ya utangazaji, Mediaset.

Haijulikani kazi atakayoifanya Berulsconi kama adhabu yake ya huduma kwa jamii lakini duuru nchini humo zinasema kuwa huenda akafanya kazi katika makao ya kuwahudmuia watu wenye ulemavu.

Bilionea huyu amekuwa akikumbwa na kesi nyingi mahakanai kutokana na kashfa mbali mbali.