Maombi ya Arsene Wenger yajibiwa

Image caption Man City 2-2 Sunderland

Maombi ya kocha ,wa Arsenal Arsene Wenger ya kuitaka Everton ishindwe ilikuisaidia timu yake kufuzu kwa kombe la mabingwa msimu ujao yalitimia hapo jana ,Crystal Palace ilipoilaza Everton mabao 3-2 na

kuiruhusu Arsenal kusalia katika nafasi ya nne ikiwa na alama 67 alama moja zaidi ya Everton.

Wenger ambaye ameshuhudia timu yake ikidorora kutoka nafasi ya kwanza mwezi januari hadi ya tano mapema juma hili amesema hiyo ndiyo ombi lake kuu ya kuhakikisha Arsenal inamaliza katika nafasi ya nne bora na kufuzu

kwa ligi kuu ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Crystal Palace 3-2 Everton

Katika mechi nyingine iliyochezwa jana usiku ,azimio la Manchester City kutwaa kombe la ligi hiyo ya Uingereza yalipata pigo baada ya timu hiyo kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Sunderland.

Bao la kwanza lilipachikwa wavuni na Fernandinho kunako dakika ya 2.

Man City 2-2 Sunderland

Sunderland ilisawazisha kunako dakika ya 73 na kuongeza lingine dakika kumi baadaye kupitia kwa mchezaji Wikham.

Nasri ndiye aliyemuokoa kocha Manuel Pelligrini aibu ya kushindwa alipofunga bao la kusawazisha kunako dakika ya 88 ya mechi hiyo.

Kutokana na matokeo hayo Pelligrini sasa anategemea matokeo ya vinara wa ligi hiyo Liverpool na Chelsea kubaini matumani yake ya kutwaa taji la mwaka huu.

The Reds ndio wanaoongoza jedwali la ligi na alama 77 ikifuatiwa na Chelsea ikiwa na alama 75.

Man city inashikilia nambari ya tatu kwa alama 71.