Pistorius:Ushahidi wa mtaalamu wazua utata

Haki miliki ya picha .
Image caption Kesi dhidi ya Pistorius inatarajiwa kuahirishwa hadi Mei tarehe tano

Mtaalamu wa uchunguzi wa mauaji anahojiwa vikali na mwendesha mkuu wa mashitaka katika kesi ya mauaji dhidi ya mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius.

Picha za risasi zilizomuua Reeva Steenkamp alizopiga Roger Dixon zilikinzana na zilie zilizopigwa na polisi na mtaalamu mwingine wa mauaji waliokuwa mashahidi wa upande wa mashitaka.

Pistorius alikana kumuua mpenzi wake Reeva kwa makusudi mwezi Februari mwaka jana.

Aliambia mahakama kuwa alifyatua risasi baada ya kuhisi kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka unasema kuwa Pistorius alimuua mpenzi wake aliyekuwa na miaka 29 baada ya wawili hao kuzozana

Huenda Oscar akafungwa jela miaka 25 au kifungo cha maisha ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake kwa makusudi.

Kesi hiyo inatarajiwa kuahirishwa hadi tarehe 5 mwezi Mei.

Roger Dixon, ni shahidi wa upande wa utetezi, na katika ushahidi wake alisema kuwa Steenkamp alikuwa anasimama karibu na mlango na risasi zote nne zilimgonga hadi akaanguka sakafuni kinyume na ushahidi wa upande wa mashitaka ulivyosema nkuwa Pistorius aligeuka katika sehemu alipokuwa na kuendelea kumpiga risasi Steenkamp.

Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani anasema kuwa ushahidi wa bwana Dixon unakinzana na ule wa upande wa mashitaka unaosema kuwa Steenkamp alikuwa na muda wa kupiga mayowe baada ya kupigwa risasi ya kwanza na kisha Pistorius akaendnelea kumpiga risasi.