Utulivu warejea huko Bor Sudan Kusini

Haki miliki ya picha Reuters

Jeshi la Sudan kusini limesema kuwa hali imetulia katika mji wa Bor ,siku mbili baada ya takriban watu 48 kuuawa katika shambulizi la raia waliokuwa katika kambi ya vikosi vya umoja wa mataifa.

Hatahivyo mapigano yanaendelea katika maeneo mengine ya taifa hilo.

Waasi wanasema kuwa wameiteka miji pamoja na maeneo ya mafuta katika jimbo la Unity.

Hatahivyo madai hayo yamekanishwa na jeshi la Sudan Kusini.

Kiongozi wa waasi Riek Machar amesema kuwa vikosi vyake vitayalenga maeneo ya mafuta ambayo ndio chanzo kikubwa cha mapato ya serikali.