Mkenya na Mmarekani washinda Boston

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Meb Keflezighi mshindi wa mbio za wanaume

Bingwa mtetezi wa mbio za Boston Marathon, Rita Jeptoo ameshinda mbio za Boston Marathon upande wa wanawake kwa saa mbili dakika 18 wakati Meb Keflezighi akinyakuwa ushindi upande wa wanaume kwa saa mbili 2 dakika nane.

Meb Keflezighi amekuwa mmarekani wa kwanza kushinda mbio hizo katika miaka 30.

Mbio hizo zilifanyika katika mazingira ya ulinzi mkali hasa kutokana na shambulizi la mwaka jana mwishoni mwa mbio hizo lililowaua watu 3 na kuwajeruhi mamia.

Waandalizi walidhibiti usalama kutokana na idadi kubwa ya washiriki ambo idadi yao ilikuwa elfu 36.

Jamaa wa waathiriwa wa shambulizi la mwaka jana pia walipewa nafasi ya kushiriki mbio hizo zilizositishwa mwaka jana baada ya shambulizi kutokea.

Buzunesh Deba wa Ethiopia alimaliza wa pili upande wa wanawake kwa muda wa saa 2 dakika 19 .