Mustakabali wa Moyes Man U

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Nini mustakabali wa Moyes Man U?

Klabu ya Manchester United inasema kuwa David Moyes hajafutwa kazi lakini imekataa kuzungumzia mstakabali wa kocha huyo katika klabu hiyo.

Magazeti nchini Uingereza yanasema kuwa klabu hiyo huenda ikamfuta kazi Moyesa kufuatia msururu wa matokeo mabaya msimu huu.

Hata hivyo msemaji wa klabu hiyo alithibitisha kuwa Moyes bado hajafutwa kazi.

Alipohojiwa kuhusu ikiwa kocha huyo ataaga klabu hiyo kabla ya mwisho wa msimu,alijibu kwa kusema kawaida hawazungumzii utabiri.

Hakuna hata gazeti moja limesema kuwa Moyes amefutwa kazi.

Jarida la Daily Mail limenukuliwa likisema kuwa Moyes huenda akafutwa kazi kabla ya msimu kuisha wakati Daily Telegraph likisema amepoteza uungwaji mkono wa wamiliki wa klabu hiyo na huenda akafutwa kazi.

Moyes aliteuliwa na Sir Alex Ferguson, kumrithi kama meneja wa klabu hiyo alipostaafu baada ya kuhudumu kama meneja kwa miaka 26

Moyes mwenye umri wa miaka 50, alipewa mkataba wa miaka sita na kuondoka Everton kuongoza mabingwa wa ligi lakini mkataba wake huenda unaelekea ukingoni baada tu ya miezi kumi.