Mkuu wa Facebook awashauri wanawake

Haki miliki ya picha
Image caption Sheryl Sandberg ni mwanamke mwenye cheo cha juu zaidi katika kampuni ya Facebook

Mwanamke anayeshikilia cheo cha juu zaidi katika kampuni ya Facebook, amewataka wanawake kuchukua hatua za kubuni mazingira ya usawa kote duniani.

Sheryl Sandberg, afisaa mkuu wa mipango katika Facebook, amesema kuwa wanawake, wanapaswa kushikilia nafasi muhimu katika biashara.

"ikiwa unatafakari kuhusu kufanya kitu, jiulize nini unachoweza kufanya ikiwa hauna uoga na basi ukifanye,'' Bi Sheryl aliambia BBC.

Sandberg ni mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo katika kampuni hiyo tangu mwaka 2012.

Mwaka jana aliandika kitabu kwa jina 'Lean In' ambacho kinawashauri wanawake kuhusu wanavyoweza kupiga hatua katika nafasi zao za kazi.

"ni muhimu sana kwamba wanawake ambao ni nusu ya idadi ya watu wote, waanze kushikilia vyeo katika meza za maamuzi , lakini bado hatujafika hapo, '' alisema .

Alisema kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi muhimu sana katika biashara,serikali ni pamoja na kuwa wajasiri amali

Akizungumzia baadhi ya changamoto zinazokumba Facebook, Sandberg alisema kuwa dunia inashuhudia mageuzi makubwa ya kiteknolojia ambayo yanahusisha simu ya rununu na Facebook ipo katikati ya mageuzi hayo