Marekani yaonya Urusi kuhusu vikwazo

Haki miliki ya picha AP
Image caption Marekani inadai kuwa Urusi inachochea vurugu nchini Ukraine

Marekani imeonya Urusi dhidi ya matamshi yake makali kuhusu Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo John Kerry ameitaka Urusi kupunguza ukali wa matamshi yake kuhusu Ukraine la sivyo iwekewe vikwazo zaidi.

Kadhalika imetaka nchi hiyo ishurutishe vikosi vinvayounga mkono Urusi nchini Ukraine kuweka chini silaha.

Serikali ya mpito ya Ukraine inasema kuwa nchi za Magharibi pamoja na serikali ya Urusi zinawaamuru wapiganaji hao kuendelea na vita chini Ukraine. Madai ambayo Urusi imekanusha vikali.

Maafisa wakuu wa Ukraine wameanzisha tena kampeini dhidi ya ugaidi katika miji kadhaa hasa eneo la Mashariki linalodhibitiwa na wanajeshi wanaounga mkono Urusi.

Rais wa muda wa Ukraine, Olexander Turchynov , aliamuzu kuanzishwa kwa operesheni hiyo baada ya wanaume wawili akiwemo mwanasiasa Vladimir Rybak - kupatikana wakiwa wameuawa kinyama.