Ryan Giggs azungumzia Man U

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Giggs ametajwa kama meneja wa muda wa Manchester

Ryan Giggs amefanya mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kama meneja wa muda wa timu ya soka ya Manchester United kufuatia kufutwa kazi kwa David Moyes mapema wiki hii .

Ameelezea siku chache zilizopita zimekuwa kama fujo tupu kwa klabu hiyo na akaahidi kujaribu kurejesha tabasamu kwenye nyuso za mashabiki .

Hii ni kufuatia kufutwa kazi kwa meneja wa klabu hiyo David Moyes kutokana na matokeo mabaya ya klabu hiyo katika ligi ya Premier.

Alianza kwa kumshukuru Meneja wa zamani Moyes kwa kumpatia fursa ya kwanza kufanya kazi kama kocha.