Obama awasili Korea Kusini kushauriana

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Obama akifanya mashauriano na Rais wa Korea Kusini, Park Geun-hye (kushoto) na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe.

Rais Obama amewasili Korea Kusini huku hofu ikizagaa kwamba Korea Kaskazini huenda inajiandaa kufanya jaribio la nne ya zana zake za nukyla.

Inatarajiwa kwamba shughuli mpya katika kinu cha nuklya mjini Pyongyang zitatawala mazungumzo kati ya bwana Obama na rais wa Korea Kusini Park Geun-hye.

Viongozi hao wawili wanarajiwa kuangazia zaidi jukumu la Uchina katika kuithibiti Korea Kaskazini, jambo ambalo Bwana Obama ametaja kuwa lenye umuhimu mkubwa.

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili Korea Kusini katika sehemu yake ya pili ya ziara katika Bara la Asia. Anatarajiwa kukutana na Rais Park baadaye leo na kuwatembelea wanajeshi wa Marekani walioko nchini humo.

Ziara yake inafanywa wakati ambapo kuna hofu kuwa Korea Kaskazini huenda ikafanya jaribio la nne la Kinukilia.

Korea Kaskazini inatarajiwa kujadiliwa na viongozi hao wawili na tayari kuna ripoti kuwa maandalizi ya kufanya jaribio la Kinukilia yanayoendelea kufanywa Korea Kaskazini yatahakikisha kuwa taifa hilo jirani linapewa kipao mbele katika mashauriano.

Picha zilizochukuliwa na mitambo ya Sattelite zinaonyesha kuwa kuna masanduku mengi yanayohamishwa hapa na pale katika eneo linalotarajiwa kufanyiwa zoezi hilo Korea Kaskazini.