Afisaa mkuu wa UN azuru Sudan Kusini

  • 29 Aprili 2014
Image copyright
Image caption Vurugu zinashuhudiwa nchini Sudan pande za kisiasa zikizozana kuhusu mamlaka

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu , Navi Pillay yuko nchini Sudan kusini kutathmin hali huko baada ya miezi minne ya mzozo .

Ziara yake inakuja siku kadhaa tu baada ya watu wenye silaha kushambulia kambi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Bor, na kuwauwa takriban watu 58 wakiwemo wahudumu na watoto .

Bi Pillay atakutana pia na watu walioyahama makazi yao kutokana na vita. Juma lililopita mamia ya raia waliuawa Bentiu-- mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa Mafuta .

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini , Barnaba Mariel Benjamin ameiambia BBC kuwa serikali yake inataraji Umoja wa Mataifa utalaani mauaji ya raia wanayolaumiwa kuyafanya waasi .

Wakati huo huo wawakilishi wa pande husika na mzozo huo wamerejea mjini Addis Ababa Ethiopia kufufua mazungumzo ya amani