Real Madrid yafuzu kwa fainali

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Real madrid yafuzu kwa fainali ya kombe la mabingwa bara Uropa

Vigogo wa ligi kuu ya Uhispania Real Madrid, wamekuwa timu ya kwanza kufuzu kwa fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya baada ya kuinyeshea Mabingwa watetezi wa kombe hilo Bayern Munich ya Ujerumani kwa mabao manne kwa nunge na hivyo kuibuka a ushindi mkubwa wa jumla ya mabao 5-0.

Sergio Ramos alifunga mabao mawili mapema katika kipindi cha kwanza cha mechi hiyo.

Kabla ya nyota wa Ureno na mchezaji bora duniani Christiano Ronaldo kuihakikishia Madrid fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 2002 na mkwaju wa wa freekick.

Bao hilo lilikuwa lake la 16 katika ligi ya mabingwa barani Uropa.

Kwa Bayern, kichapo hicho kilikuwa ni kama wembe wa kutu kwao kwani mwaka uliopita Wajerumani hao waliifunga Barcelona 7-0 katika hatua ya nusu fainali kabla ya kuilaza Borussia Dortmund na kutwaa taji lao la tano barani ulaya.

Haijulikani kufikia sasa iwapo halmashauri inayoingoza klabu hiyo itachukua hatua yeyote dhidi ya kocha wa klabu hicho Pep Guardiola ambaye licha ya kuiongoza Barca kutwaa taji la Bundesliga ameshindwa kutetea hadhi ya klabu

hiyo katika mchuano huu wenye kitita kikubwa zaidi.

Madrid sasa inasubiri kujua iwapo itachuana na Chelsea ya Uingereza chini ya ukufunzi wake aliyekuwa kocha wao Jose mourinho ama wapinzani wao wa mji wa Madrid , Athletico .

Mshambulizi wa Athletico Madrid Diego Costa alisema anatumai Chelsea hawata regesha basi kwenye lango lao ilhali watacheza mchezo yenye maarifa.

Timu hizo zilitoka sare tasa katika mkondo wa kwanza .