IMF:Urusi yaingia mdororo wa uchumi

Haki miliki ya picha r
Image caption Mgogoro wa Ukraine watishia uchumi wa Urusi

Shirika la Fedha Duniani, IMF, limesema Urusi kwa sasa imeingia katika kipindi cha "mdororo wa uchumi" kutokana na hasara iliyosababishwa na mgogoro wa Ukraine.

Shirika hilo, ambalo limeshusha makadirio yake ya kukua kwa uchumi wa Urusi, limesema nchi hiyo mwaka huu itapoteza dola bilioni 100.

Mkuu wa ujumbe wa IMF nchini Urusi, Antonio Spilimbergo, amesema vikwazo vya kimataifa vinaharibu uchumi wa Urusi na kutishia uwekezaji.

Uchumi wa Urusi, ulisinyaa katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.

Lakini Bwana Spilimbergo amesema anatarajia hali hiyo kuendelea.

"Kama unaelewa mdororo wa robo mbili za kushuka kwa uchumi, basi ufahamu Urusi inakabiliwa na mdororo kwa sasa," amesema Bwana Spilimbergo.

Shirika la IMF limeshusha makadirio yake ya kukua kwa uchumi wa Urusi mwaka 2014 kutoka asilimia 1.3% hadi asilimia 0.2% na kusema kwamba Shirika hilo linatarajia uchumi wa Urusi kukua kwa asilimia 1% tu mwaka unaofuata.