Hodgson kutaja kikosi cha Uingereza

Image caption Kocha wa Uingereza Roy hogson kutaja timu ya kombe la Dunia

Kocha wa timu ya Uingereza Roy Hodgson atakitaja kikosi cha taifa kitakachoshiriki katika kombe la dunia litakaloandaliwa mwezi juni Brazil.

Hodgson atataja kikosi hicho kitakacho shirikisha wachezaji 23 na wachezaji 7 wa akiba kabla ya kutaja kikosi chake cha mwisho tarehe mbili Juni.

Uingereza imeratibiwa kuchuana dhidi ya a Peru tarehe 30 Mei katika mechi ya kujipima nguvu .

Timu hiyo vilevile imepangiwa kushiriki mechi zaidi za kirafiki dhidi ya kabla ya Honduras na Ecuador mjini Miami Marekani.

Uingereza iliyojumuishwa katika kundi D itafungua kampeni yake katika dimba la kombe la dunia tarehe 14 Juni dhidi ya Italia kisha ielekee Sao Paulo tarehe 19 Juni kumenyana na Uraguay kisha imalize udhia dhidi ya Costa Rica tarehe 24 Juni.

Mchezaji wa Uingereza anayechezea klabu ya Tottenham, Andros Townsend hatashiriki katika kombe la dunia baada ya kupata jereha katika kifundo cha mguu wake hapo jana.