Mwanasiasa maarufu akamatwa N. Ireland

Image caption Kiongozi wa Sinn Fein Gerry Adams amekamatwa

Polisi huko Ireland Kazkazini wamemkamata mwanasiasa mashuhuri wa chama cha Sinn Fein ,Gerry Adams kwa kuhusishwa na mauaji yaliyotokea yapata zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Adams anahojiwa kuhusu mauaji ya Jean McConville ambaye alitekwanyara na kundi la waasi la IRA mnamo mwaka 1972 na kisha akapatikana amepigwa risasi na kuuawa .

Kiongozi huyo amekanusha kuhusika kivyovyote vile akisema kuwa alijipeleka binafsi kuzungumza na polisi ilikujaribu kusuluhisha madai hayo yaliyomwandama kwa miaka mingi mno .

Adams anakanusha kuhusika kwa vyovyote vile na utekaji nyara wala mauaji yake bi McConville ambaye alikuwa mama wa watoto kumi .

Adams anazuiliwa kutokana na kifo cha mjane huyo aliyetekwa nyara na kundi la IRA mwaka wa 1972 .

Madai haya yanafwatia mahojiano mjini Belfast mwaka wa 2001-2006 baina ya chuo kikuu cha Boston Marekani na wakereketwa wa vita hivyo vilivyonuiwa kuikomboa Ireland kutoka kwenye minyororo ya ukoloni.

Image caption Kiongozi wa Sinn Fein Gerry Adams amekamatwa

Mahojiano hayo yalifanywa kwa misingi kuwa mahojiano hayo yangewekwa siri hadi baada ya vifo vya wahusika wakuu,lakini baada ya kesi za kutaka kutambulika wahusika na wahasiriwa waliotoweka wakati wa vita hivyo

chuo hicho kililazimishwa kutoa sehemu ya mahojiano kwa serikali ya Ireland.

Mmoja kati ya watu 16 waliosemekana kutoweka ni bi McConville .

Mjane huyo alilaumiwa na IRA kuwa mpelelezi wa polisi lakini baada ya ufafanuzi wa polisi yapata mwaka wa 1999, McConville ilibainika kuwa hakuwa.

Kundi hilo la IRA lilikiri kutekeleza mauaji yake bi McConville mwaka wa 1999 lakini mwili wake ulipatikana mwaka wa 2003 ukiwa umetupwa kwenye ufukwe wa bahari.

IRA inashtumiwa kwa kampeini na mauaji yaliyotikisa Ireland kaskazini kwa takriban miaka thelathini.