Meya mlevi wa Toronto

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meya Rob Ford

Meya mwenye utata wa mji wa Toronto, Rob Ford amesema kuwa atachukua mapumziko ya muda ili kutatua tatizo lake la ulevi.

Mwanasheria wa Meya huyo Dennis Morris amesema mteja wake anaelewa kuwa ana tatizo linalomdhalilisha na anataka kuchukua hatua kulitatua.

Tangazo lake linajiri wakati ambapo magazeti mawili ya Canada yanasema yamepata kanda mpya ya video yenye kutia aibu ya Bwana Ford.

Katika kanda hizo Bwana Ford anaonekana akitumia mihadarati aina ya cocaine akiwa amelewa chakari huku nyengine akionekana akitoa matamshi mabaya kuhusu wanawake na wanasiasa wenzake katika baa moja.

Mkanda huo wa video unamwonyesha katika miezi ya hivi karibuni akiwa amelewa.

Mwaka uliopita Bwana Ford alikiri kuwa alikuwa akitumia mihadarati akiwa meya baada ya kukataa kwa miezi kadhaa kuvuta midarati hiyo wakati anapolewa ambapo pia alipinga wito wa kumtaka ajiuzulu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meya Rob Ford akicheza kwenye ukumbi wa jiji la Toronto wimbo wa Bob Marley One Love

Pia polisi wana malalamiko kwa njia ya maandishi kuwa meya huyo amekuwa akituhumiwa akitumia lugha ya matusi, akiwatishia wafanyakazi wenzake, akiwadhalilisha wanawake na kutumia mihadarati akiwa kwenye mgahawa. Tuhuma ambazo meya huyo amezikana.

Meya huyo sasa anataka kugombea tena nafasi hiyo mnamo mwezo Octoba,lakini anasema kwamba atapumzika kwa muda katika kampeni zake za umeya ili kutatua tatizo lake la ulevi.