Putin ataka Ukraine kuonda majeshi

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Urusi Vladmir Putin na Chansela wa Ujerumani Angela Markel.

Rais wa Urusi, Vladmir Putin, ametoa wito kwa Ukraine iyaondoe majeshi yake katika maeneo ya Kusini Mashariki mwa taifa hilo na kuanza mazungumzo kama njia mojawapo ya kusuluhisha mgogoro unaoendelea nchini humo.

Ofisi ya Rais imesema kuwa wito huo ulitolewa katika mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na kiongozi wa Ujerumani, Chansela Angela Markel.

Taarifa hiyo ilisema kiongozi wa Ujerumani alimpigia simu Bwana Putin akimwomba asaidie kuwaachilia wachunguzi wa Jumuiya ya Ulaya wa OSCE wanaozuiliwa na wanamgambo wanaoiunga mkon Urusi walipo Ukraine Mashariki.

Wachunguzi hao 12, kukiwemo raia watano wa Ukraine, walitiwa mbaroni na wapiganaji hao wanaounga mkono Urusi katika mji wa Mashariki wa Sloviansk.