Mwaka 1 kuitafuta ndege ya Malaysia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Meli inayohusika katika shughuli za kuitafuta nfege ya Malysia MH370

Maafisa wanaoongoza juhudi za kuitafuta ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea ikiwa njiani kwenda China, wamesema kuwa shughuli ya kuitafuta huenda ikachukua hadi mwaka mmoja.

Akiongeza na wandishi wa habari nchini Malaysia, afisa mkuu Angus Houston alisema kuwa ana Imani kuwa msako wa mwaka mmoja utaweza kutegua kitendawili cha ndege hiyo.

Maafisa nchini Australia, China na Malaysia, watakutana mjini Canberra wiki ijayo, kujadili juhudi za kusaka mabaki ya ndege hiyo ambazo bado zinaendelea

Mnamo siku ya Alhamisi, kulikuwa na taarifa kwamba ndege ya MH370 ilianza kutafutwa baada ya saa nne za kupotea kwake.

Ripoti ya hapo awali kutoka kwa waziri wa usafiri wa Malysia, pia ilisema kuwa wahudumu wa trafiki ya ndege, hawakugundua kuwa ndege hiyo ilitoweka hadi dakika kumi na saba baada ya kukosa kuonekana katika mtambo wa Radar.

Ndege hiyo ilikuwa imewabeba watu 239 ilipotoweka ikiwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China njiani kuelekea Beijing.