Watoto saba wauawa kinyama Honduras

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi wa Honduras wa kupambana na mahadarati na magenge ya uhalifu

Serikali nchini Honduras inachunguza vifo vya watoto saba ambao huenda waliuawa baada ya kukataa kujiunga na magenge ya uhalifu katika mji wa viwanda wa San Pedro Sula.

Siku ya alhamisi ,Polisi walifanikiwa kupata mwili wa mtoto wa miaka saba ambaye mwili wake ulioneka kuwa alikuwa ameteswa kabla ya kuuawa.

Kaka ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 pia alikutwa amekufa siku kadhaa zilizopita.

Mwanasheria Mkuu nchini Honduras Oscar Chinchilla yupo katika mji huo ili kusimamia uchunguzi huo.

Taifa hilo la Honduras lina idadi kubwa ya matukio ya mauaji duniani ambapo inakadiriwa watu 15 wamekuwa wakiuawa kwa siku, takwimu hizo ni kwa mujibu ya mamlaka ya nchi hiyo.