Mashambulizi yatanda nchini Misri

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption wafuasi wa Jenerali Abdel Fatah Al sisi

Kumekuwa na misururu ya ghasia nchini Misri ,siku moja tu kabla ya kuanza rasmi kwa kampeni za uchaguzi wa urais mwezi huu.

Mashambulizi mawili ya walipuaji wa kujitoa muhanga kusini mwa Sinai yamemuua mwanajeshi mmoja na kuwajeruhi watu saba siku ya ijumaa.

Afisa mmoja aliuawa katika shambulizi la bomu mjini Cairo,huku watu wawili wakiuawa kwa kupigwa risasi katika mji wa bandari wa Alexandria wakati wafuasi wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi walipokuwa wakikabiliana na wakaazi .

Wanamgambo wameimarisha mashambulizi yao dhidi ya vikosi vya usalama licha ya kuwepo kwa msako dhidi ya waislamu wenye itikadi kali na wanajeshi wa serikali.

Waandishi wanasema kuwa aliyekuwa kiongozi wa jeshi Abdel Fattah Al sisi ambaye mwaka uliopita alimuondoa madarakani Mohammed Morsi anatarajiwa kushinda kwa wingi wa kura.