Mlipuko wa bomu waua sita Somalia

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Askari wa zimamoto akizima moto uliotokana na bomu lililolipuka kwenye gari

Watu wanaokadiriwa kufikia sita wakufa kutokana na mlipuko mkubwa wa bomu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Mwandishi wa habari wa BBC katika mji huo anasema watu sita akiwemo kiongozi wa zamani wa serikali ya mtaa ni miongoni mwa waliokufa.

Mlipuko huo uliotokea karibu na katikati mwa mji umesabbaishwa na bomu lililotegwa kandokando ya barabara.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Al Shabaab

Mashambulizi katika mji wa Mogadishu yamekuwa yakiongezeka kwa kipindi cha miezi ya hivi karibuni.

Mashambulizi mengi yamekuwa yakitekelezwa na kundi la wanamgambo wa Al Shaabab, ambalo linakabiliana na operesheni kubwa kutoka kwa vikosi vya umoja wa Afrika AMISOM kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya Somalia.

Kundi hilo limejiondoa kwenye miji mingi lakini bado lina nguvu linashikilia miji kwenye maeneo ya vijijini ya Kusini na Katikati mwa Somalia.