Ukraine yawaachia waangalizi wa OSCE

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waangalizi wa OSCE walioachiliwa huru

Waangalizi 7 wa kimataifa waliokamatwa siku nane zilizopita na wanaharakati wanaounga mkono Urusi,wamewachiliwa huru,pamoja raia watano wa Ukraine waliokuwa nao.

Kiongozi wa kundi la raia wa Ukraine wanaotaka kujitenga na taifa hilo mjini Sloviansk Vyacheslav Ponomaryov ,ameelezea kwamba waangalizi hao ni wageni wake na kwamba wamewachiliwa bila vikwazo.

Urusi imekuwa chini ya shinikizo ya mataifa ya magharibi kuwaachilia huru waangalizi hao ili kupunguza hali ya wasiwasi mashariki mwa Ukraine.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Waangalizi wa kimataifa OSCE waliokuwa wakishikiliwa Ukraine

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo amesema kuwa waanfgalizi hao waliweza kuachiliwa huru kupitia mjumbe mmoja wa Urusi Vladmir Lukin.