Je ANC ni maarufu kuliko Rais Zuma?

Kampeni za uchaguzi katika nchi yoyote ile zinachosa sana.

Lakini Mmusi Maimane mmoja wa waliojitokeza katika kampeni za uchaguzi wa Urais nchini Afrika Kusini, anakabiliana na mambo mengi zaidi ya koo yake iliyomkauka.

Dhana yake ni kwamba upinzani nchini Afrika Kusini hauna fursa ya kuiondoa mamlakani serikali ya Afrika Kusini baada ya miaka 20 mamlakani.

‘‘Ni vigumu sana, ni kampeini ngumu mno,’’ anasema Mmusi mwenye umri wa miaka 33 na ambaye pia ni msemaji wa chama cha upinzani cha Democratic Alliance, akiwa na hisia mseto pamoja na kuonekana kuishiwa na uvumilivu anapozungumzia nguvu za chama tawala ANC.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Hellen Zile anayegombea Urais katika chama cha upinzani cha Democratic Alliance

Kwa maoni yake kutokana na chama cha ANC kubana matangazo ya upinzani katika kituo cha televisheni ya taifa, Maimane anasema kuwa, ‘‘chama tawala kimeanza kutumia mbinu ambazo tumekuwa tukiona katika baadhi ya mataifa ya Afrika hasa nchini Zimbabwe...huku ANC ikianza kutumia mbinu za Robert Mugabe na chama chake Zanu PF.’’

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais Zuma akiwa katika mkondo wa kampeni zake

Mnamo siku ya Jumapili, mamia walijitokeza kuhudhuria moja ya mikutano ya Rais Jacob Zuma , kiongozi wa chama tawala ANC.

Hapa ndipo kulikuwa na ishara kwamba sio wote wanaohisi kama Maimane.

Kunao wafusi wa ANC pia wanaoona mazuri ya chama hicho katika miaka 20 iliyopita.‘‘Nilikulia katika umaskini mkubwa, kwa sababu ya ANC nilifanikiwa kusoma shule bila malipo na sasa ninafanya kazi na kujikimu kimaisha. Mimi ni mmoja wa watu ambao wameweza kufanikisha ndoto zao,’’ asema Zanele Ngcobo, mwenye umri wa miaka 24.

Chama maarufu kuliko kiongozi

Rais Zuma amekabiliwa na wakati mgumu katika muhula huu unaokwisha, kashfa za ufisadi hasa kwa kutumia mali ya umma kuikarabati nyumba yake ya kifahari na uongozi duni pamoja na kuongezeka kwa viwango vya umasikini.

Lakini ambali na hayo, kura za maoni zinaonyesha kuwa ANC chini ya uoongozi wa Jacob Zuma kiko mbele kwa ushawishi kwa asimilia 60. Bila shaka ni jambo la kuwatia moyo mashabiki wake na chama ambacho kimekuwa kikikabiliwa na tuhuma si haba.

Sasa je inakuwaje kuwa chama cha ANC kinaendelea kuwa maarufu? Tafakari mambo haya!

Ni ukweli kuwa waafrika weusi nchini humo wako katika hali nzuri kuliko ilivyokuwa mwaka 1994.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Chama cha ANC kinasemekana kuwa maarufu kuliko kiongozi wake

Chama cha ANC kina mizizi ya ukombozi wa waafrika weusi.

Mamilioni ya waafrika weusi wanaoishi katika umasikini, wanategemea mfumo ambao unaonekana kujali masilahi yao.

Na kwa kuwa hapajakuwa na chama kingine mamlakani tangu kukamilika kwa enzi ya ubaguzi wa rangi, basi wengi wanaona chama cha ANC kama cha pekee kinachoweza kuendelea kuwasaidia.

Maisha yamebadilika kwa baadhi ya waafrika weusi. Wameanza kumiliki mali, kupata kazi kubwa kubwa na kuwa katika hali nzuri ya maisha. Kwao hawana haja ya kupinga mfumo, uko sawa tu.