Hukumu ya wanajeshi wabakaji DRC leo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa serikali ya DRC

Hukumu inatarajiwa kutolewa baadaye leo kwenye kesi inayowahusu wanajeshi 39 wanaotuhumiwa kuendesha ubakaji na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Wanajeshi hao wanatuhumiwa kusababisha machafuko yanayoendelea kwenye mji mdogo wa Minova ulio mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2012.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waasi wa M23 ambao wanadaiwa nao kujihusisha na vitendo vya ubakaji

Wakati wa machafuko hayo maelfu ya wajeshi wa serikali walikuwa wakirudi nyuma baada ya kupoteza mji wa Goma kwa waasi wa M23 .

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa wanajeshi hao waliwabaka karibu wanawake na wasichana 135.

Matukio ya ubakaji yameenea katika eneo la mashariki mwa Congo na yanaidiwa kufanywa na askari wa pande zote mbili waasi na wale serikali.