Giggs: Msife moyo Man U itarejea

Image caption Giggs awaasa mashabiki wa Man United Ufanisi utarejea

Kaimu kocha wa Manchester United Ryan Giggs amewarai mashabiki wa klabu hiyo maarufu kuwa wasife moyo ushindi utarejea Old Trafford katika siku za usoni.

Kigogo huyo wa Manchester United aliwaasa mashabiki punde baada ya kuingoza Manchester united kuilaza Hull city mabao 3-1 katika mechi yao ya mwisho ya nyumbani msimu huu wa ligi kuu ya premia ya Uingereza.

Hiyo ndiyo iliyokuwa mechi yake ya mwisho baada ya kushiriki mechi 963 akivalia jezi la Man united.

Kaimu kocha huyo mwnye umri wa miaka 40 alifunga ukurasa wa kipindi chake huko Old Trafford kwa kumkaribisha uwanjani kizazi kijacho cha wachezaji wa timu hiyo alipomkaribisha chipukizi James Wilson.

Tineja huyo alifunga mabao mawili kabla ya Robin van Persie kutamatisha kichapo hicho.

Image caption Mashabiki wamuomba Giggs asiondoke Man United

Bao la kufutia machozi la Hull lilifungwa na Matty Fryatt.

Kufuatia matokeo duni ya United msimu huu timu hiyo inaweza kufuzu kushiriki mchuano wa kuwania ubingwa wa taji la Europa iwapo watailaza Southampton na kuomba kuwa Tottenham ikunguwae katika mechi yao ya nyumbani dhidi ya Aston Villa. Mechi hiyo itakuwa siku ya Jumapili. Hadi kufikia sasa, kocha Louis van Gaal ndiye anayepigiwa upatu kuchuakua hatamu kama mkuu wa kiufundi Old Trafford ijapokuwa tangazo rasmi linasubiriwa wakati wowote kabla ya mechi dhidi ya Southampton.