Francois Bozize kuwekewa vikwazo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kulia;Ni aliyekuwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize.

Wajumbe katika Umoja wa Mataifa wanasema kuwa wamekubaliana kumuwekea vikwazo aliyekuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize pamoja na watu wengine wawili wanaotuhumiwa kusababisha mzozo unaondelea nchini humo.

Bwana Bozize ambaye aliondolewa madarakani na waasi wa kiislamu wa Seleka mwaka uliopita,Nourredine Adam-kiongozi wa waasi wa Seleka na Levy Yakete ambaye aliiwaongoza wanamgambo wa kikristo wataorodheshwa miongoni mwa watu wabaya zaidi duniani.

Wanakabiliwa na marufuku ya kutosafiri pamoja na kupigwa tanji kwa mali zao.

Umoja wa mataifa umeonya kutokea kwa mauaji ya kimbari nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ambapo maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani wameshindwa kusitisha mashambulizi ya kulipiza kisasi kati ya waislamu na wakristo.