Watu 200 kushtakiwa nchini Misri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwendesha mashtaka mkuu nchini Misri

Mwendesha mashtaka nchini Misri amewafungulia mashtaka watu 200 wanaodaiwa kuwa wanachama wa kundi moja la waislamu wenye itikadi kali kutokana na misururu ya mashambulizi dhidi ya vitengo vya usalama.

Hatahivyo hakuna terehe iliotolewa ya kuanza kusikizwa kwa kesi dhidi ya wanachama hao wa kundi la Ansar Bet Al maqdis.

Takriban wanacham 100 wa kundi hilo ambao kesi zao ziko tayari kuanza hawajulikani waliko.

Kundi hilo limekiri kutekeleza mashambulizi kadhaa , mengi yakifanywa baada ya kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi.

Maafisa wamelishtumu kundi la Muslim Brotherhood kwa kupanga ghasia hizo madai ambayo yamepingwa na kundi hilo.